MAMBO YA KUSHANGAZA KUHUSU KIFO.
MAMBO YA KUSHANGAZA KUHUSU KIFO. Kifo limekuwa jambo lenye kuogopwa na wengi kiasi kwamba siku hizi imekuwa nadra sana kuzungumziwa na watu, lengo lao likiwa ni kujifariji na kujisahaulisha kuwa siku moja watakufa. Hali hii imepewa jina kitaalamu inaitwa 'Thanatophobia' neno lenye maana "hofu ya kifo." Watalamu wa mambo ya saikolojia wamebainisha kuwa kwa kawaida kimtishacho binadamu ni kile asichokijua (Fear of the unknown), hali hii pia inaitwa Xenophobia. Hivyo wengi hukiogopa kifo kwa sababu hawakijui. Kuufahamu ukweli kuhusu kifo kutakusaidia kuendelea kuwa jasiri na kukuondolea hofu iliyojengeka ndani yetu kuhusu hatma ya kila mmoja wetu. KIFO NI NINI? Kuna nadharia nyingi sana kuhusu kifo. Nyingi kati ya nadharia hizo zimejikita zaidi katika masuala ya kidini na kiimani. Taarifa tulizonazo kisayansi kuhusu kifo ni kidogo sana hivi kwamba maswali yaliyopo ni mengi kuliko majibu. Kitabu Reasoning From The Scriptures kinaeleza kuwa kifo, "ni kukoma kwa ...