YAJUE MACHACHE KUHUSU TATIZO SUGU LA KUKOSA USINGIZI (Fatal insomnia)
Tatizo sugu la kukosa usingizi. Binafsi nimekuwa mtu ambaye inapofika majira ya usiku hasa wakati wa kulala inakuwa vigumu mno kupata usingizi wa kueleweka. Baada ya kupitia hali hii siku kadhaa nikaona ulazima wa kuchunguza tatizo hili ili nifahamu undani wake na namna nitakavyoweza kulikabili. Katika pita pita zangu za hapa na pale mtandaoni nikakutana na simulizi moja ya kusikitisha sana iliyokuwa na kichwa kilichosomeka, "You fall asleep only when You Die." Simulizi hiyo ni tukio la kweli kabisa lililotokea mwaka 1991 linamhusu bwana mmoja aliyeitwa Michael A. Corke raia wa marekani aliyekuwa na umri wa miaka 40. Bwana huyu alikuwa mwalimu aliyekuwa akifundisha sanaa ya muziki katika shule moja ya sekondari huko Chicago. Alianza kupata mashaka kutokana na dalili zisizo za kawaida alizoanza kuziona kwenye ulalaji wake. Tofauti na matatizo ya kawaida anayokutana nayo mtu aliye na shida ya kupata...