YAJUE MACHACHE KUHUSU TATIZO SUGU LA KUKOSA USINGIZI (Fatal insomnia)
Tatizo sugu la kukosa usingizi.
Binafsi nimekuwa mtu ambaye inapofika majira ya usiku hasa wakati wa kulala inakuwa vigumu mno kupata usingizi wa kueleweka. Baada ya kupitia hali hii siku kadhaa nikaona ulazima wa kuchunguza tatizo hili ili nifahamu undani wake na namna nitakavyoweza kulikabili. Katika pita pita zangu za hapa na pale mtandaoni nikakutana na simulizi moja ya kusikitisha sana iliyokuwa na kichwa kilichosomeka, "You fall asleep only when You Die." Simulizi hiyo ni tukio la kweli kabisa lililotokea mwaka 1991 linamhusu bwana mmoja aliyeitwa Michael A. Corke raia wa marekani aliyekuwa na umri wa miaka 40. Bwana huyu alikuwa mwalimu aliyekuwa akifundisha sanaa ya muziki katika shule moja ya sekondari huko Chicago. Alianza kupata mashaka kutokana na dalili zisizo za kawaida alizoanza kuziona kwenye ulalaji wake. Tofauti na matatizo ya kawaida anayokutana nayo mtu aliye na shida ya kupata usingizi kama vile kuamka mara nyingi nyakati za usiku au kulala usingizi wa mang'amung'amu, Bwana huyu yeye hakuwa akipata usingizi hata kidogo! Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo hali ya bwana Corke ilivyozidi kuwa mbaya. Alianza kupata matatizo ya kimwili na kihisia kama vile kuona ukungu, kizunguzungu na kukosa usawaziko alipotaka kutembea. Taratibu alianza kuonyesha dalili za ugonjwa wa akili. Kuna wakati alianza kuona mambo kama yuko njozini, na mambo ambayo hayakuwepo. Mwishowe alipoteza utambuzi wa kutofautisha kile alichokiona kwenye akili yake na kile kilichokuwepo kwenye ulimwengu halisi.Baada kupelekwa hospitali, Corke alikuwa ameathiriwa vibaya sana na tatizo hilo kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kufanya chochote. Akawa akitegemea familia yake imfanyie kila kitu, alikuwa hawezi hata kuvaa nguo na kuoga. Alikuwa hawezi kuwasiliana, afya yake ikadhoofika kwa kasi mno. Awali madaktari walidhani pengine alikuwa na tatizo liitwalo Multiple Sclerosis ugonjwa unaotokana na kuharibika kwa vifuniko vya neva zilizo kwenye ubongo na ungwe-uti. Hali ambayo huzuia mtiririko wa taarifa ndani ya ubongo wenyewe, na kati ya ubongo na mwili. Madaktari wakashangaa kwani jamaa hakuonyesha dalili zozote zilizoendana na ugonjwa huo wa Multiple Sclerosis. Muda si mrefu madaktari hao waligundua hali isiyo ya kawaida kuhusu ulalaji wa bwana Corke. Usiku alikuwa akifumba macho kana kwamba amelala lakini walipomfanyia kipimo cha Electroencephalogram au EEG katika ubongo wake, walishangaa kipimo hicho kilipoonyesha kuwa ubongo wake haukuwa ukilala hata kidogo licha ya kuwa alikuwa amefumba macho akiashiria kulala. Hili ndilo tatizo linalojulikana kama Fatal Insomnia lililokuwa likimsumbua bwana huyu. Pamoja na kugundua tatizo lililokuwa likimtesa bwana huyo madaktari walishindwa kumsaidia kutokana na ukweli kuwa hapakuwa na tiba wala dawa ya kutibu ugojwa huo. Baada ya miezi 6 Michael A. Corke alifariki kutokana na tatizo hilo. Tatizo hilo lilimfanya awe macho kwa muda wa wiki 24 sawa na miezi 6 hali iliyopelekea kifo chake.
Mtu akifanyiwa kipimo cha Electroencephalogram.
FATAL INSOMNIA NI NINI?
Kitaalamu ni shida ambayo inaaminika kutokana na chembe za protini zilizo kwenye ubongo ziitwazo prion ambazo huathiri eneo la ubongo liitwalo Thalamus, eneo ambalo ni mahususi kwa kuratibu na kutupatia usingizi tunapolala. Eneo hilo linapoharibiwa matokeo yake huwa tatizo sugu la kukosa usingizi. Dalili za tatizo hilo huanza polepole na kukua hatua kwa hatua hatimaye huwa mbaya. Kwa kawaida mgonjwa aliye na fatal insomnia hufariki ndani ya miezi 7 hadi 73 tangu alipoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huu. Watu walio kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ni wale walio na wastani ya miaka 40.
FATAL INSOMNIA NI NINI?
Kitaalamu ni shida ambayo inaaminika kutokana na chembe za protini zilizo kwenye ubongo ziitwazo prion ambazo huathiri eneo la ubongo liitwalo Thalamus, eneo ambalo ni mahususi kwa kuratibu na kutupatia usingizi tunapolala. Eneo hilo linapoharibiwa matokeo yake huwa tatizo sugu la kukosa usingizi. Dalili za tatizo hilo huanza polepole na kukua hatua kwa hatua hatimaye huwa mbaya. Kwa kawaida mgonjwa aliye na fatal insomnia hufariki ndani ya miezi 7 hadi 73 tangu alipoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huu. Watu walio kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ni wale walio na wastani ya miaka 40.
Tangu kisa hicho cha kusikitisha kiliporekodiwa mwaka 1991 mpaka leo hii haijapatikana tiba ya ugonjwa huu. Ajabu ni kuwa mgonjwa aliye na fatal insomnia hata anapopewa vitulizo vilivyo na nguvu kubwa ya kumfanya mtu alale usingizi mzito kama Barbiturate na Benzodiazepine bado dawa hizo hushindwa kumfanya mgonjwa alale usingizi. Kitu ambacho madaktari hukifanya ni kujaribu kupunguza madhara ambayo hutokana na dalili za ugonjwa na si kutibu ugonjwa wenyewe.
Baada ya kusoma kisa hicho cha kusikitisha mwili wangu ulisisimka kwa woga nikajikuta nikiyakumbuka maneno aliyowahi kuyaandika Nabii Musa hapo zamani. "Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu ninayemtumaini. Kwa maana utaniokoa nisinaswe na ugonjwa unaoangamiza. Nami nitapata kimbilio chini ya mabawa yako". Zaburi 91:2-4...



Maoni
Chapisha Maoni